Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 22:29

Watu 25 wauwawa Palestina na mashambulizi ya Israel


Wapalestina wakitathmini uharibifu kufuatia shambulizi la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, Julai 6, 2024. Picha ya AFP
Wapalestina wakitathmini uharibifu kufuatia shambulizi la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, Julai 6, 2024. Picha ya AFP

Takriban watu 25 wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya shambulizi la anga Jumanne kwenye shule iliyogeuzwa makazi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao, kwa mujibu wa maafisa wa afya wa Palestina.

Shambulizi la Jumanne, ambalo ni lanne la Israeli katika siku kadhaa, lilipiga lango la shule ya al-Awda huko Abasan, karibu na mji wa kusini wa Khan Yunis. Jeshi la Israel limesema linachunguza ripoti hiyo.

Pia lilifuatiwa na mashambulizi matatu ya awali ambayo Israel imekiri kuwa yalilenga wanamgambo wa Hamas waliojificha katika maeneo ya raia.

Wizara ya afya ya Gaza imeripoti kuwa shambulizi la Israel la Jumamosi liliuwa watu 16 katika shule ya al-Jawni inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa mjini Nuseirat, katikati mwa Gaza, ambapo takriban watu 2,000 walikuwa wamejihifadhi.

Forum

XS
SM
MD
LG