Waziri wa Mambo ya Ndani Suleyman Soylu akizungumzia mafuriko hayo amesema Jumapili kati ya waliofariki mmoja wao ni afisa wa polisi ambaye gari lake lilisombwa na maji.
Akitembelea mji wa Dereli, katika mkoa wa Giresun, Soylu alisema watu 127 wameokolewa na kuwa barabara zinazoelekea katika vijiji 118 katika eneo hilo la mafuriko zimefungwa.
Picha za Televisheni zilionyesha magari na vifusi vikielea katika barabara kuu ya Dereli iliyoko takriban kilomita 20 kutoka pwani.
Mvua kubwa Jumamosi jioni ililazimisha kuokolewa watu katika nyumba za ghorofa baada ya maporomokoya ardhi kutokea katika mkoa wa Rize, kilomita 180 mashariki ya Giresun.
Kwa mujibu wa Kituo cha kutabiri hali ya hewa, mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha huko Giresun na mikoa iliyoko jirani ya Trabzon, Rize na Artvin lat.