Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:29

Tetemeko la Ardhi : Idadi ya waliokufa Uturuki yafikia 39


Waokoaji wakiwa wanamtoa mwanamke kutoka katika kifusi cha jengo baada ya tetemeko kupiga katika mji wa Elazig, mashariki ya Uturuki, Jan. 25, 2020.
Waokoaji wakiwa wanamtoa mwanamke kutoka katika kifusi cha jengo baada ya tetemeko kupiga katika mji wa Elazig, mashariki ya Uturuki, Jan. 25, 2020.

Kitengo cha kushughulikia maafa Uturuki kimesema Jumatatu idadi ya waliokufa kufuatia tetemeko la ardhi lenye nguvu imeongezeka kufikia 39.

Takriban watu 4,000, ambao walikuwa wakisaidiwa na mashine za kuchimbia, wamekuwa wakifanya shughuli ya kuchakua kifusi katika baridi ya barafu huko Elazig upande wa mashariki wa nchi hiyo baada ya tetemeko lenye ukubwa wa 6.8 kilichopiga Ijumaa jioni.

Maafisa wanasema majengo 76 huko Elazig yalianguka na mamia mengine yaliharibika.

Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa wafanyakazi wanaotoa msaada wa dharura wamejenga mahema 9,500 ili kuweza kuwapatia chakula na malazi watu waliohama makazi yao.

Serikali imesema kuwa hadi sasa wamefanikiwa kuwatoa watu 45 kutoka katika kifusi.

Televisheni ya Uturuki imeonyesa mama mmoja, Ayse Yildiz, 35, na mtoto wake wa kike, 2, Yusra akiokolewa kutoka katika mabaki ya nyumba iliyokuwa imebomoka huko katika mji wa Elazig. Walikuwa wamekwama ndani ya jengo hilo lililoanguka kwa masaa 28.

Mwanafunzi katika chuo kikuu cha Syria Mahmud al Osman ameliambia shirika la habari la serikali Anadolu kuwa alitumia mikono yake kumuokoa mwanaume na mwanamke kutoka chini ya kifusi.

Kitengo cha usimamizi wa maafa na huduma za dharura kimesema Zaidi ya watu 1,600 walikuwa wamejeruhiwa kutokana na tetemeko hilo, kati yao 13 wakiwa katika hali mbaya wakipata matibabu katika kitengo cha wagonjwa wenye hali mbaya.

XS
SM
MD
LG