Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:00

Maandalizi ya mazishi ya Rais Mugabe yakamilika


Marehemu Rais Mugabe
Marehemu Rais Mugabe

Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe unatarajiwa kuwasili Jumatano Zimbabwe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe mjini Harare. 

Mugabe, 95, alifariki dunia wiki iliyopita akiwa hospitalini nchini Singapore baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters taarifa ya serikali ilitumwa kwenye ofisi za ubalozi Jumapili na kusema ibada ya mazishi ya Mugabe itafanyika katika uwanja wa taifa wa michezo mjini Harare siku ya Jumamosi na mazishi siku moja baadae.

Taarifa zilieleza kuwa wakuu wa nchi mbalimbali watakaohudhuria maombolezo hayo wataondoka mara moja kwa sababu maafisa wa serikali ya Zimbabwe watakuwa na shughuli nyingi za maandalizi ya mazishi hayo.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG