Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:35

Wazimbabwe wamtaka Mugabe ajiuzulu


Maandamano ya kushinikiza Mugabe kujiuzulu Zimbabwe
Maandamano ya kushinikiza Mugabe kujiuzulu Zimbabwe

Wakati hatma ya utawala wa Rais Mugabe ukiwa bado umegubikwa na maamuzi ya kisiasa, maelfu ya raia wa Zimbabwe wameonekana Jumamosi mitaani wakiongeza shinikizo kuwa ajiuzulu.

Vyanzo vya habari mjini Harare vinasema kuwa raia hao walikuwa wakijiandaa kwa mkutano unaoungwa mkono na chama tawala ZANU-PF ikiwa ni kuendeleza kampeni hiyo dhidi ya Mugabe wakinyoosha mabango yao juu yakisema Mugabe lazima aachie madaraka (Mugabe Must Go).

Zanu-PF ndiyo chama kilichomsaidia Mugabe kuingia madarakani miaka 40 iliyopita, lakini hivi sasa wamerudi nyuma kufuatia mpasuko wa kisiasa unaoendelea kujitokeza nchini humo.

Duru za kisiasa zinasema kitendawili juu ya nani atakaye kuwa mrithi wa Rais Mugabe pale atapofikia uamuzia wa kuachia madaraka kimeendelea kutanda duniani kote.

Hivi karibuni Jeshi la nchi hiyo limedaiwa kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani na wamekuwa wakifanya mazungumzo kutafuta ufumbuzi juu suala hilo wakidai kuwa walikuwa wakiwalenga wahalifu na siyo Mugabe na familia yake.

Baadhi ya ripoti za vyombo vya habari vimesema Mugabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfukuza kazi wiki iliyopita.

Pia kuna taarifa kuwa uhasama baina ya makamu wa rais na mkwe Mugabe uliotokana na kupigania madaraka.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Mugabe ameeleza nia yake ya kuendelea na uongozini mpaka wakati ambapo chama chake kitakapofanya mkutano mwezi ujao.

XS
SM
MD
LG