Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:11

Tillerson ahimiza utawala wa kiraia Zimbabwe


Rais Robert Mugabe akiwa na Jenerali Constantino Chiwenga ikulu mjini Harare, Zimbabwe, Novemba 16, 2017.
Rais Robert Mugabe akiwa na Jenerali Constantino Chiwenga ikulu mjini Harare, Zimbabwe, Novemba 16, 2017.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson ametoa wito Ijumaa Zimbabwe kurejea katika utawala wa kiraia.

Shirika la habari la AP limeripoti kuwa Tillerson amesema Zimbabwe bado inayofursa ya kuanza "utaratibu mpya" wakati kuna dalili kuwa uongozi wa mabavu wa Robert Mugabe utalazimishwa kuachia madaraka katika mapinduzi yaliyofanyika bila ya kumwaga damu.

"Sisi sote lazima tushirikiane ili kurejesha kwa haraka utawala wa kiraia katika nchi hiyo kwa mujibu wa katiba, Tillerson aliuambia mkusanyiko wa mawaziri wa mambo ya nje na wanadiplomasia waliokusanyika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Amesema ni lazima Zimbabwe ifanye uchaguzi uliyo huru na haki. Mugabe alishinda katika chaguzi zilizopita ambazo wasimamizi waliokuwepo wakati wa uchaguzi huo waligundua kuwa ulivurugwa.

“Mwisho wa yote wananchi wa Zimbabwe ni lazima wapewe fursa ya kuchagua serikali yao,” aliongeza

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ameonekana Ijumaa hadharani kwa mara ya kwanza leo Ijumaa, tangu jeshi la nchi hiyo kumzuilia nyumbani kwake siku ya Jumatano, kuchukua udhibiti wa taasisi za serikali na kuanziisha mazungumzo yanayotarajiwa kumruhusu baba wa taifa kustahafu.

Kiongozi huyo mkongwe, akiwa amevaa kofia na mavazi ya rangi ya samawati na manjano, alihudhuria sherehe ya kuhitimu wanafunzi elfu moja katika chuo kikuu, mjini Harare, huku akishangiliwa na umati wa watu.

Wazimbabwe wanatumai kwamba mzozo wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo utatatuliwa kwa haraka, huku viongozi wa upinzani, wanaharakati na viongozi wa kidini wakimtaka Mugabe kuondoka madarakani, baada ya jeshi kuchukua udhibiti wa serikali.

Hata hivyo, ripoti zilieleza kuwa Mugabe hajasalimu amri. Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliliambia bunge la nchi yake kwamba ni mapema mno kuchukua msimamo wowote kuhusiana na mzozo huo.

XS
SM
MD
LG