Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:34

Mugabe atoa dukuduku baada ya 'mapinduzi' Zimbabwe


Rais Emmerson Mnangagwa
Rais Emmerson Mnangagwa

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe ametoa dukuduku lake kwa mara ya kwanza tangu aondolewe madarakani katika kile alichokiita ni 'mapinduzi ya kijeshi' yaliomuondoa kwenye madaraka mwaka 2018.

Kiongozi huyo wa zamani Robert Mugabe amesema hajawahi kufikiria kwamba Rais mpya Emmerson Mnangagwa atamgeukia na amelaani kitendo cha kumuondoa madarakani, katika mahojiano na Shirika la habari la Reuters.

Mugabe, 94, ameiongoza Zimbabwe tangu kupata uhuru mwaka 1980 mpaka aliposhinikizwa kuachia madaraka na washirika wa Mnangagwa walioko katika jeshi la nchi hiyo Novemba mwaka 2018.

Mugabe kwa baadhi ya watu ni shujaa kutokana na harakati za ukombozi wa nchi hiyo, lakini wengine wanamkumbuka Mugabe kwa kusababisha uchumi wa Zimbabwe uliokuwa imara kuharibika na nchi hiyo kutengwa kimataifa.

Mnangagwa, aliyekuwa makamu wa rais chini ya Mugabe, ameahidi kukaribisha wageni kuja kuwekeza nchini humo na pia kurejesha mahusiano na nchi za Magharibi baada ya kuchukua madaraka.

“Sikufikiria kabisa kwamba mtu ambaye nimemjenga na kumleta katika serikali na juhudi kubwa niliofanya kuokoa maisha yake alipokuwa jela alipokuwa ametishiwa kunyongwa, kwamba siku moja atakuwa ndiye mtu atanigeukia,” Mugabe amesema katika mahojiano na shirika la utangazaji la Serikali la Afrika Kusini SABC akiwa Harare.

Mnangagwa alihukumiwa kunyongwa kwa kosa la uhujumu chini ya utawala wa wazungu waliowachache. Lakini alisamehewa kunyongwa kwa sababu ilionekana kuwa alifanya kosa hilo wakati akiwa mtoto mdogo.

Mugabe amesema aliondolewa madarakani “katika mapinduzi ya kijeshi” na kuwa Mnangagwa alichukuwa urais kinyume cha sheria.

XS
SM
MD
LG