Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:17

Kwa nini zoezi la kuhesabu kura linachukuwa muda mrefu Marekani?


Wafanyakazi wa Uchaguzi Marekani wakipitia karatasi za kura katika ofisi za Uchaguzi za Kaunti ya Clackamas, May 19, 2022, Mjini Oregon, Ore.
Wafanyakazi wa Uchaguzi Marekani wakipitia karatasi za kura katika ofisi za Uchaguzi za Kaunti ya Clackamas, May 19, 2022, Mjini Oregon, Ore.

Uwiano wa madaraka katika Bunge la Marekani  kufuatia uchaguzi wa katikati ya muhula Jumanne bado haujafikia tamati, huku uchaguzi katika maeneo kadhaa  muhimu bado hakuna matokeo  saa 48 baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa.

Mtindo wa kusubiri matokeo mbalimbali kwa siku kadhaa ni wa kawaida hapa nchini Marekani, ambako ni vyombo vya habari kwa kawaida hutangaza matokeo ya awali, kulingana na majumuisho ya kura yanayofanywa na makarani na maafisa wengine pamoja na uchambuzi za takwimu.

Wakati uchelewesho wa muda mrefu unaweza kuwachukiza wapiga kura wa Marekani – na kuibua maswali kutoka kwa wafuatiliaji wa kimataifa – kuna sababu kadhaa kwa nini mchakato huo unaweza kuchukua muda mrefu.

Kwa kuanzia, uchaguzi wa Marekani uko katika himaya ya majimbo kwa sehemu kubwa, na kila jimbo kati ya majimbo 50 lina kanuni zake.

Baadhi ya Wamarekani wanatumia mashine kupiga kura; wengine, wanatumia karatasi za kupiga kura. Baadhi wanapiga kura vituoni; wengine wanapiga kura kwa njia ya posta.

Baadhi wanapiga kura Siku ya Uchaguzi. Wengine wanapiga kura mapema. Raia wengi wa Marekani hutumia fursa ya kupiga kura katika masanduku ya kupiga kura yaliyoko mitaani.

Wakati maafisa wa uchaguzi katika majimbo kadhaa wakiwasihi watu kuwa na subira huku kura zikihesabiwe, Seneta Mrepublikan Marco Rubio wa Florida ametangaza malalamiko yake.

Marco Rubio
Marco Rubio

“Iwapo Florida inaweza kuhesabu kura milioni 7.5 katika saa 5 kwa nini inachukua siku kadhaa kwa baadhi ya majimbo kuhesabu kura zisizozidi milioni 2?” Rubio alituma ujumbe wa Twitter Jumatano.

Karatasi za Kura mbalimbali, ambazo kwa kawaida Wamarekani wanatumia kupiga kura kwa wagombea tofauti na masuala mbalimbali, zinaweza kuchukua muda kuzihesabu.

Huku upigaji kura kwa njia ya posta ukiwa umepata umaarufu kote nchini wakati wa janga la COVID-19, vitu vinachukua muda mrefu zaidi – kura zinaweza kufika katika vituo vya kuhesabu kura siku kadhaa baada ya uchaguzi. Ohio na Alaska wanahesabu kura zinazowafikia hadi siku 10 baadae.

Ikiwa ni mchanganyiko wa mambo kadhaa, katika majimbo mengi, maafisa wa uchaguzi hawaruhusiwi hata kuanza kuhesabu mapema kura zinazowasili kwa njia ya posta.

Muda zaidi unaohitajika kutekeleza mchakato huo unachochea nadharia za hujuma mbalimbali, hususan baada ya uchaguzi wa mwaka 2020, ambapo Rais Donald Trump alisema uongo akidai uchaguzi ulichakachuliwa dhidi yake..

Ushindani kati ya Trump na hatimaye ushindi wa Joe Biden ulijulikana baada ya siku nne.

XS
SM
MD
LG