Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 05:17

Kupunguza ndege zisizo na rubani Niger huenda kukaathiri operesheni dhidi ya ugaidi


Wanajeshi wa Ufaransa wakipakia makombora kenye ndege isiyo na rubani katika kituo cha anga kilichopo Niamey, Niger. Picha na Malaury Buis/EMA/DICOD/AP.
Wanajeshi wa Ufaransa wakipakia makombora kenye ndege isiyo na rubani katika kituo cha anga kilichopo Niamey, Niger. Picha na Malaury Buis/EMA/DICOD/AP.

Maafisa wawili wa Marekani wameiambia VOA kwamba safari za ndege za kijeshi zisizokuwa na rubani kutoka kambi za kijeshi nchini Niger zimekuwa "chache" tangu mapinduzi ya Julai, wataalam wa vikwazo wanaamini huenda vikadumaza mpango wa kimataifa wa kukabiliana na ugaidi Afrika Magharibi.

Maafisa hao walizungumza na Sauti ya Amerika wiki hii kwa sharti la kutokutajwa majina yao ili kujadili maswala nyeti ya kiusalama.

Wizara ya Ulinzi wa Marekani imesita kuzungumzia masuala mahususi ya operesheni zake za usalama na za kukabiliana na ugaidi, zaidi ya kusema kwamba jeshi la Marekani limesitisha "ushirikiano wa kiusalama" na Niger kutokana na mabadiliko ya kisiasa.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi, Brigadia Jenerali Pat Ryder amekiri kwa waandishi wa habari kwamba hali ya Niger " dhahiri” u si “ya kawaida” kwa jeshi la Marekani, akiongezea kwamba uwepo wa jeshi hilo nchini Niger bado haujabadilika, wakati Marekani ikiwa na matumaini ya suluhu ya kidiplomasia kuumaliza hali hiyo.

Niger ni kitovu cha jeshi la Marekani kwa kukabiliana na ujasusi, na ugaidi, upelelezi, na uchunguzi huko Afrika Magharibi. Eneo hilo limekuwa likipambana na makundi kadhaa ya wanamgambo yakiwemo makundi ya Islamic State na Jama'a Nusrat ul-Islam wa al-Muslimin, yenye makao yao nchini Mali na kufanya harakati zao Afrika Magharibi.

Maafisa wa sasa na wa zamani wa Marekani wameonyesha wasiwasi kwamba upungufu wa upelelezi na ufuatiliaji utaathiri juhudi za kimataifa kuvisaidia vikosi vya usalama vya ndani kupambana na taasisi za kigaidi.

Jeshi la Marekani linaweza kurusha ndege zisizo na rubani kutoka mji mkuu wa Niger, Niamey, na limeanzisha kituo kingine cha anga kilicho umbali wa mamia ya kilomita, huko Agadez, ili kupanua wigo wake wa uchunguzi na upelelezi katika eneo tete la Bonde la Ziwa Chad lililopo katika nchi za Cameroon, Chad, Niger na Nigeria. Tangu 2019, Marekani imekuwa ikitumia mpango huo wa ndege zisizo na rubani katika masuala ya kijasusi, upelelezi, na uchunguzi.

Kupunguza operesheni hizo kuna "athari kubwa" kwa uwezo wa jeshi kufanya operesheni za kukabiliana na ugaidi, kwa mujibu wa Jenerali Mstaafu wa Wanamaji Frank McKenzie, kamanda wa zamani wa operesheni za kijeshi za Marekani katika Mashariki ya Kati.

Forum

XS
SM
MD
LG