Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:40

AU yasimamisha uanachama wa Niger


Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat

Umoja wa Africa – AU  umesimamisha uanachama wa Niger katika shughuli zake zote kufuatia mapinduzi ya kijeshi huko na kuwaambia wanachama wake kuepuka hatua zozote zinazoweza kuhalalisha  utawala wa kijeshi Niger.

Mapinduzi ya mwezi uliopita yamezusha wasi wasi miongoni mwa washirika wa Magharibi na nchi za kidemokrasia za Afrika ambazo zinahofia kwamba hatua hiyo inaweza kuyaruhusu makundi ya Kiislamu yenye harakati zake katika eneo la Sahel na kupanua uwepo wao na kuipa Russia nafasi ya kuongeza ushawishi wake.

Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi- ECOWAS imekuwa ikijaribu kufanya mashauriano na utawala wa kijeshi lakini imesema iko tayari kutuma wanajeshi Niger kurejesha utaratibu wa kikatiba kama juhudi za kidiplomasia zitashindikana.

Baraza la amani na usalama la AU limesema katika taarifa yake Jumanne kwamba inazingatia uamuzi wa kuliweka tayari jeshi la ECOWAS na kuiomba tume ya AU kutathmini matokeo ya kiuchumi , kijamii na kiusalama ya kupeleka jeshi kama hilo.

Maazimio katika taarifa ya Jumanne yalipitishwa kwenye mkutano wa baraza uliofanyika Agosti 14 .

Viongozi wa jeshi mbalimbali wakiwa na wajumbe wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi.
Viongozi wa jeshi mbalimbali wakiwa na wajumbe wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi.

Ecowas inataka kuachiliwa haraka rais Mohamed Bazoum aliyekamatwa tangu wakati wa mapinduzi .

Chanzo cha habari hii ni mashirika mbalimbali ya habari

Forum

XS
SM
MD
LG