Hatua hiyo imependekezwa kuchukuliwa iwapo diplomasia itashindwa kurejesha uongozi wa kidemokrasia, kufuatia mapinduzi ya kijeshi.
Maafisa wa kijeshi walimwondoa madarakani Rais wa Niger Mohamed Bazoum mnamo Julai 26, na wamekaidi wito wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika Magharibi ECOWAS, na wengine, wa kumrejesha kazini, na hivyo kufanya mataifa yenye nguvu za kikanda kuamuru kikosi maalum kuundwa.
Wakati wa mkutano huo, wakuu wa ulinzi wamekuwa wakijadili vifaa na mambo mengine, yanayohusu uwezekano wa kupelekwa kwa wanajeshi nchini Niger, kulingana na ratiba rasmi.
Utumiaji wa nguvu unasalia kuwa suluhisho la mwisho, lakini "ikiwa kila kitu kingine kitashindwa, vikosi mashujaa vya Afrika Magharibi ... viko tayari kujibu mwito wa wajibu," Kamishna wa ECOWAS wa Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama, Abdel-Fatau Musah alisema, mwanzoni mwa hafla hiyo siku ya Alhamisi.
Alisema nchi nyingi kati ya 15 wanachama wa Umoja huo zimejiandaa kushiriki katika kikosi maalum, isipokuwa zile ambazo pia ziko chini ya utawala wa kijeshi - Mali, Burkina Faso na Guinea - na Cape Verde.
Forum