Shirika la masuala ya kibinadamu la Umoja huo, OCHA, limesema kwamba hata kabla ya rais wa taifa hilo aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Bazoum kuondolewa madarakani, tayari taifa hilo lilikuwa na zaidi ya watu milioni 3 waliokuwa bila usalama wa chakula.
Wengine milioni 7 ambao hali hao ilikuwa nafuu kidogo huenda wakafikia viwango vya ukosefu wa usalama wa chakula kabisa, iwapo hali itaendelea kama ilivyo, OCHA imeongeza, ikitaja uchambuzi uliofanywa na shirika la chakula duniani, WFP.
Bazoum mwenye umri wa miaka 63 alizuiliwa Julai 26 na kundi la walinzi wake, yakiwa mapinduzi ya 5 tangu Niger kujipatia uhuru wake kutoka kwa Ufaransa hapo 1960. WFP imesema kwamba inaendelea kupeleka chakula kwenye taifa hilo la Sahel lisilo na bandari, licha ya hali ya kisiasa iliyopo.
Forum