Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 26, 2024 Local time: 01:25

UNHCR yaonya kuwa mzozo wa Niger huenda ukapelekea janga la kibinadamu


Polisi wa Niger wakipiga doria kwenye mji mkuu wa Niamey. August 27, 2023. Picha ya AFP
Polisi wa Niger wakipiga doria kwenye mji mkuu wa Niamey. August 27, 2023. Picha ya AFP

Wakati kukiwa hakuna suluhisho la kisiasa linaloonekana, shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi UNHCR limeonya kuwa mzozo wa Niger huenda ukapelekea janga la kibinadamu.

Hayo yamesemwa wakati kukiwa na mashambulizi kutoka makundi yenye silaha yasio ya serikali pamoja na vikwazo vilivyowekwa na ECOWAS kwenye taifa hilo lisilo na bandari.

Tangu kuondolewa madarakani kwa rais Mohamed Bazoum, aliyechaguliwa kidemokrasia hapo Julai 26, kumekuwa na hali ya taharuki, amesema mwakilishi wa UNHCR nchini Niger Emmanuel Gignac.

Ameongeza kusema kwamba ni vigumu kubashiri hali itakavyokuwa, na kwamba UNHCR na UN wameweka mikakati ya kukabiliana na dharura inayoweza kutokea.

Amesema kwamba ghasia na mashambulizi kutoka kwa makundi yenye silaha na hasa karibu na mpaka wa Mali na Burkina Faso yamesababisha zaidi ya watu 20,000 kuondoka makwao ndani ya mwezi mmoja uliopita.

Forum

XS
SM
MD
LG