Oligui "ataunda taasisi za mpito", Ulrich Manfoumbi Manfoumbi, msemaji wa Kamati ya Mpito na Marejesho ya Taasisi (CTRI) alisema kwenye kituo cha Television cha serikali siku ya Alhamisi, siku moja baada ya maafisa wa waasi kumpindua Rais Ali Bongo Ondimba.
Hakuna maelezo yaliyotolewa juu ya muda wa taasisi hizo za mpito.
Wakati huo huo viongozi wa Afrika siku ya Alhamisi wamekuwa wakitathmini jinsi ya kuwajibu maafisa wa jeshi nchini Gabon ambao alimuondoa madarakani Rais Ali Bongo na kumweka jenerali kuwa mkuu wa nchi, hili ni moja ya wimbi la mapinduzi ya hivi karibuni katika nchi za Afrika Magharibi na Kati, na kwamba mamlaka za kikanda zimeshindwa kuyabadili.
Unyakuzi huo umeumaliza utawala wa ukoo wa rais Bongo uliokuwa madarakani kwa takriban miongo sita na kuzua kitendawili kipya kwa kanda hiyo ambayo imekuwa ikitatizwa na kukabiliana na mapinduzi nane kuanzia mwaka 2020. Rais wa Nigeria aliyechaguliwa hivi karibuni alikiita kitendo hicho kuwa ni "ugandamizaji wa demokrasia."
Kambi ya kisiasa ya Afrika ya Kati, Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika ya Kati (ECCAS), yaliyalaani mapinduzi hayo katika taarifa, ikisema imepanga mkutano "unaokaribia" kufanyika wa wakuu wa nchi ili kuamua jinsi ya kujibu. Haikutoa tarehe.
Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika litakutana Alhamisi kujadili mapinduzi hayo, msemaji wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika alisema.
Maafisa wakuu wa Gabon walitangaza mapinduzi yao Jumatano kabla ya kupambazuka, muda mfupi baada ya chombo cha uchaguzi kutangaza kuwa Bongo alikuwa ameshinda muhula wa tatu kiuraini, baada ya kura zilizopigwa Jumamosi.
Jumatano jioni , iliibuka video ya Bongo iliyozuiliwa ndani ya makazi yake, akiwaomba msaada kutoka kwa washirika wa kimataifa lakini alionekana kutojua kinachoendelea karibu yake. Maafisa hao pia walimtangaza Jenerali Brice Oligui Nguema, mkuu wa zamani wa walinzi wa rais, kuwa amechaguliwa kuwa mkuu wa nchi.
Tukio hili linafuatia mapinduzi yaliyofanyika miaka minne iliyopita nchini Mali, Guinea, Burkina Faso, Chad na Niger, baada ya mafanikio ya kidemokrasia tangu miaka ya 1990 na kuibua wasiwasi miongoni mwa mataifa ya kigeni yenye maslahi ya kimkakati ya kikanda.
Mapinduzi hayo pia yalionyesha uwezo mdogo wa mataifa ya Afrika mara baada ya jeshi kuchukua madaraka. ECOWAS ilitishia kuweka vikwazo na kutumia nguvu za jeshi kuingilia kati mapinduzi Niger, baad aya mapinduzi hayo kutokea Julai 26, lakini junta haijarudi nyuma.
Viongozi wa kijeshi kutoka nchi mbalimbali pia wamekuwa wakipinga kwa kutoa shinikizo la kimataifa kwa nchi kama vile Mali. Lakini maafisa hao wa jeshi wameweza kushikilia madaraka na wengine hata kuungwa mkono na kupata umaarufu.
Chanzo cga habari hii ni Shirika la habari la Reuters/ AFP
Forum