Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:22

Maafisa waasi huko Gabon wametangaza kuchukua madaraka nchini humo

Maafisa waasi nchini Gabon wakitangaza kuchukua nchi na kusitisha matokeo ya uchaguzi
Maafisa waasi nchini Gabon wakitangaza kuchukua nchi na kusitisha matokeo ya uchaguzi

Maafisa waasi katika taifa lenye utajiri wa mafuta la Gabon wametangaza Jumatano kuwa wamekamata madaraka kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata ambapo Rais Ali Bongo Ondimba, aliyekuwa madarakani tangu mwaka 2009, alitangazwa mshindi.

Bongo mwenye umri wa miaka 64, ambaye familia yake imeitawala Gabon kwa zaidi ya miaka 55 amewekwa kwenye kifungo cha nyumbani na mmoja wa watoto wake wa kiume alikamatwa kwa uhaini, viongozi wa mapinduzi wamesema.

Katika hotuba ya kushangaza kabla ya uchaguzi, kundi la maafisa lilitangaza taasisi zote za jamhuri zimevunjwa, matokeo ya uchaguzi yamefutwa na mipaka kufungwa.

Leo, nchi inapitia mgogoro mkubwa wa kitaasisi, kisiasa, kiuchumi na kijamii, kulingana na taarifa hiyo iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa. Taarifa ilisomwa na afisa aliyeandamana na darzeni ya makanali, wanachama wa kikosi Republican Guard, wanajeshi wa kawaida na wengine.

Forum

XS
SM
MD
LG