Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:16

Wapiga kura nchini Gabon wajielekeza kwenye vituo vya kupigia kura kumchagua rais mpya na wabunge


Watu wakisubiri kwenye foleni kufunguliwa kwa kituo cha kupigia kura katika uchaguzi wa rais mjini Libreville, Agosti 26, 2023.
Watu wakisubiri kwenye foleni kufunguliwa kwa kituo cha kupigia kura katika uchaguzi wa rais mjini Libreville, Agosti 26, 2023.

Wapiga kura nchini Gabon leo Jumamosi wamekwenda kwenye vituo vya kupigia kura kumchagua rais mpya, wabunge na wawakilishi wa serikali za mitaa, katika uchaguzi ambao wanasiasa wa upinzani wana matumaini utamaliza utawala wa zaidi ya miongo mitano wa familia ya Bongo.

Rais aliye madarakani Ali Bongo anawania muhula wa tatu. Ameiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2009. Kabla ya hapo, baba yake aliliongoza taifa hilo la Afrika ya Kati lenye utajiri wa mafuta.

Albert Ondo Ossa, mmoja kati ya wagombea 14 wa urais amesema “Gabon sio mali ya kina Bongo.”

Ondo Ossa mgombea wa muungano mkuu wa vyama vya upinzani, Alternance 2023 aliteuliwa wiki iliyopita.

Mabadiliko ya hivi karibuni kwenye sheria ya upigaji kura mwaka huu imebainika kuwa yenye utata, huku wakosoaji wakisema hatua mpya inakinufaisha zaidi chama tawala cha Gabonese Democratic.

Kutokana na mabadiliko hayo, kura kwa naibu kiongozi wa manispaa itakuwa mara moja kura kwa naibu mgombea urais.

Wakosoaji wanasema kwamba mabadiliko hayo yatafanya uchaguzi usiwe wa haki, kwa sababu mgombea wa upinzani Ossa haungwi mkono na chama kimoja pekee.

Forum

XS
SM
MD
LG