Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 20:59

ECOWAS inawaambia viongozi wa mapinduzi Niger kufikiria msimamo wao


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika magharibi (ECOWAS) na pia Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu. July 30, 2023
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika magharibi (ECOWAS) na pia Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu. July 30, 2023

Majenerali waliomuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum katika uasi wa Julai 26 wametaja kipindi cha mpito cha miaka mitatu huku Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi ikitaka kurejeshwa mara moja kwa utaratibu wa kikatiba

Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) Ijumaa iliwaambia viongozi wa mapinduzi ya Niger kuwa “hawajachelewa sana” kufikiria upya msimamo wao wakati wakizozana juu ya kurejea kwa utawala wa kiraia na chaguo la nguvu za kijeshi bado lipo mezani.

Majenerali waliomuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum katika uasi wa Julai 26 wametaja kipindi cha mpito cha miaka mitatu huku Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi ikitaka kurejeshwa mara moja kwa utaratibu wa kikatiba.

Wakati wajumbe wakisafiri kwenda mji wa Niamey, ECOWAS inasema mazungumzo bado yanaendelea kuwa kipaumbele wakati wakuu wa ulinzi wakiandaa kikosi maalum kwa uwezekano wa matumizi halali ya nguvu ili kurejesha demokrasia kama itahitajika.

Mapinduzi ya Niger yameongeza mivutano katika eneo la Sahel mahala ambako serikali nyingine tatu zimeanguka kwa uasi wa kijeshi tangu mwaka 2020 na wapiganaji wa jihadi wanadhibiti maeneo ya eneo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG