Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:12

Kongamano la Kimataifa: Biden aahidi kushirikiana na washirika wa kieneo


Rais Joe Biden akifungua kongamano la mataifa ya Amerika June 8, 2022 kwenye mji wa Los Angeles.
Rais Joe Biden akifungua kongamano la mataifa ya Amerika June 8, 2022 kwenye mji wa Los Angeles.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano amefungua kongamano la mataifa ya Amerika kwenye mji wa Los Angeles wakati akiahidi kushirikiana na washirika wa kieneo katika kutatua matatizo yanayoukabili ulimwengu.

Suala la uhamiaji lilitawala katika kikao hicho cha mataifa ya ukanda wa magharibi, wakati vongozi wengi wakilitaja kuwa na umuhimu mkubwa kwenye sera za mambo ya nje.

Rais wa Marekani alieleza kuwa: "Uhamaji wenye mpangilio na salama, ni muhimu kwa uchumi wetu ikiwemo Marekani. Unaweza kutumika kwenye maendeleo endelevu. Hata hivyo uhamiaji usio halali haukubaliki na tutahakikisha tunalinda mipaka yetu kwa ushirikiano na washirika wa kieneo.

Tumetoka mbali tangu Marekani kuwa mwenyeji wa kongamano la kwanza kama hili miaka 28 iliyopita. Azimio la kikao hicho cha kwanzakilichofanyika mjini Miami limeendelea kutoa matumaini ya kukabiliana na changamoto tulizo nazo hivi leo pamoja na uwezo mkubwa tulio nao kwenye ukanda wa magharibi katika mataifa ya Amerika."

Biden pia alitangaza ushirikiano wa kiuchumi unaolenga kuimarisha ustawi kote kwenye ukanda wa magharibi.

Rais Biden aliongeza kuwa: "Hakuna sababu yoyote kwanini ukanda wa magharibi usiwe salama, wenye maendeleo na demokrasia. Kuanzia Canada hadi Chile, tuna kila tunachohitaji. Watu wetu ni wakakamavu na pia wabunifu. Mataifa yetu yanataka kushirikiana, wakati eneo letu likishikilia familia pamoja na urafiki wa kudumu."

Baadhi ya program mpya ambazo Biden anatarajiwa kuzindua katika siku za karibuni ni pamoja na dola milioni 300 za usalama wa chakula zitakazohakikisha kuwa mataifa ya Caribbean yanapata nishati isiyo na gesi nyingi ya carbon pamoja na program ya kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya 500,000 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

XS
SM
MD
LG