Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:39

Waziri wa ulinzi wa Marekani kukutana na mwenzake wa China, Singapore


Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austine.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austine.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin pamoja na mwenzake wa China wanatarajiwa kukutana wiki hii wakati wa kikao cha masuala ya ulinzi nchini Singapore.

Mkutano huo wa moja kwa moja ni nadra kati ya viongozi wawili wa ngazi za juu kutoka serikali ya Marekani na China. Viongozi hao hata hivyo hawatarajiwi kukubaliana kuhusu masuala mengi wakati hali ya taharuki ikionekana kuendelea kupanda kati ya mataifa yote mawili.

Ripoti zinasema kwamba ndege za kijeshi za China na Russia mwezi uliopita ziliruka karibu na anga ya washirika wa Marekani huko Asia wakati rais wa Marekani Joe Biden alipokuwa kwenye ziara barani humo. Ingawa China haijaunga Russia mkono moja kwa moja kwenye vita vya Ukraine, imeonyesha ushirikiano wake na taifa hilo suala ambalo limezua wasiwasi mjini Washington.

China inachukulia Taiwan yenye demokrasia kuwa sehemu yake, wakati ikitishia kuichukua kimabavu. Rais Biden ameahidi ulinzi wa Marekani kwa Taiwan, iwapo China itajaribu kuishambulia, suala linalozua taharuki kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu duniani.

XS
SM
MD
LG