Hati mpya ya serikali inaonyesha kuwa Kenya awali ilikuwa na lengo la kuondoa kiasi cha vikwazo 7 vya nje ya ushuru (NTBs) – kanuni zenye udhibiti ikiwemo vibali, viwango vya usafirishaji, vizuizi, udhibiti wa ubadilishaji fedha za kigeni, na kuweka dhamana ya thamani ya mizigo y nchini -- katika mwaka wa fedha wa 2021/22 lakini hili lilipanda hadi 31 ikiashiria kuwepo uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili.
Kuondolewa kwa dadi ya vikwazo vya kibiashara vilivyopelekea NTBs vilitatuliwa na kuondolewa vikwazo hadi kufikia 256 ilipofika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka jana, ilitokea punde baada ya ziara ya rais Samia Suluhu nchini Kenya alipochukua nafasi ya aliyekuwa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Sera za biashara za Dkt. Magufuli za kulinda soko la ndani, mara kadhaa zimekuwa zikizua mzozo wa kidiplomasia kati ya Nairobi na Dar es Salaam.
“ Mafanikio yaliyopita kiwango yametokana na ushirikiano kati ya Kenya na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutatua vikwazo vya NTBs ili kujenga soko huria” inaeleza sehemu ya taarifa ya General Economic and Commercial Affairs Sector, kikundi kinachofanya kwa ajili ya maandalizi ya bajeti, ambayo yanaijumuisha Hazina pia.
Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa nchini Kenya