Wakizungumzia hali hiyo katika makao makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha Tanzania, baadhi ya wanahabari hao wamesema licha ya muungano huo kupiga hatua kubwa kuondoa vikwazo vya kiuchumi, bado kuna tatizo kubwa la waandishi kukosa ushirikiano wanapohitaji kupata taarifa muhimu, zikiwemo za vyanzo vya migogoro ya kisiasa inayofukuta ndani ya Jumuiya hiyo ukiwemo Unaoendelea kati ya Kongo na Rwanda, nchi ambazo zote ni mwanachama wa jumuiya hiyo.
"Naweza kusema asilimia 50 yale malengo yaliyokuwa yanatarajiwa na waanzlishi wa jumuiya yamefikiwa yameweza kutekelezwa mfano masuala yakama mahusiano ya mataifa mbalimbali ambayo yameweza kujumuhswa ndani ya jumuiya hiyo ya afrika mashariki tuko na mataifa saba," alisema Mwangi Maina, mwanahabari kutoka Kenya.
Sikiliza:
Hata hivyo Maina anasema pamoja na mafanikio hayo bado changamoto kubwa katika utoaji wa taarifa za migogoro ya kisiasa.
"Kidogo kuna vile vizingiti vinavyoletwa ma masuala ya kisasa za nchi masuala ya akidiplomasia na unakuta waandishi wanashindwa kuandika kwa sababu hawapati taarifa kwa wahusika, kumekuwa na migogoro ya nchi moja na nyingine mfano nchi ya Rwanda na Kongo kumekuwa na mvutano lakini Jumuiya haizungumzia, ilishajitokeza migogoro ya kibiashara kati ya mataifa ya Uganda na Kenya, Kenya na Tanzania, Rwanda na Uganda, lakini wahusika wakuu wakiwemo mawaziri wa nchi husika wanakuwa hawako tayari kuzungumza hawatoi taarifa ambazo ni muhimu na zinafaa kuwafikia wananchi wa jumuiya," aliongeza.
Akizungumzia changamoto hiyo mkurugenzi wa sekta za jamii wa Jumuiya hiyo Dr. Irene isakaamesema pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo wanaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo likiwemo shirika la maen deleo la ujerumani (giz)kuzitatua sambamba na kuimarisha misingi ya utoaji wa taarifa muhimu za jumuya ikiwemo ya kujenga uwezo kwa waandishi wa habari
"Jumuiya ya Afrika mashariki inafanya mambo mengi, suala kubwa ni namna ya kuwasiliana na wananchi wa kawaida waweze kuelewa kile kinachoendelea kwa sababu tunapozungumzia suala la mtangamano utekelezaji wa itifaki unategemea sera za nchi zitakazoendana na itifaki husika, kwa hiyo hapa tunahitaji watunga sera waweze kutusaidia na hapa ndio pale tunapohitaji pia wito wa kisiasa kuweza kusaidia mtangamano," alisema.
Umuhimu wa wananachi kupatataarifa na pia umezungumziwa na wadau wa maendeleo wanaosaidia jumuiya hiyo akiwemo meneja mawasiliano wa shirika la maendeleo la ujerumani (giz) Bw Marius Weist ambaye amesema wanaendelea kusaidia kutatua tatizo hilo kwa kuwajengea waandishi wa habari uwezo ili wasaidie kuwajulisha wananchi
Pamoja na Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki ambayo kwa sasa ina nchi saba wanachama kuendelea kufanikiwa kuondoa idadi kubwa ya vikwazo vya kibiashara katika a baadhi ya nchi bado inakabiliwa na baadhi ya changamoto za migogoro ambazo hata hivyo jitihada za kuitatua zinaendelea.
-Imetayarishwa na Asiraji Mvungi, VOA, Arusha