Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:10

Rwanda na DRC zafikia makubaliano kusitisha mapigano, inatarajiwa kuanza utekelezaji Ijumaa jioni


Rais wa Rwanda Paul Kagame (Kushoto), Rais wa Angola Joao Lourenco (katikati) Rais wa DRC Felix Tshisekedi (R) walipokutana kufanya mazungumzo Luanda Julai 6, 2022.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (Kushoto), Rais wa Angola Joao Lourenco (katikati) Rais wa DRC Felix Tshisekedi (R) walipokutana kufanya mazungumzo Luanda Julai 6, 2022.

Makubaliano yamefikiwa ambayo yanaweza kumaanisha ni mwanzo wa sitisho la mapigano katika eneo lililokumbwa na  ghasia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mapema ifikapo Ijumaa jioni, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Tete Antonio amesema.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi alikuwa akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta mjini Luanda Jumatano wakati mivutano ikiongezeka kati ya majirani katikati ya ghasia za umwagaji damu zinazofanywa na wanamgambo katika mipaka yao.

Eneo la mashariki mwa DRC limeshuhudia mapigano makali katika miezi ya hivi karibuni kati ya majeshi ya Congo na kundi la waasi la M23.

Makubaliano yalifikiwa kwa “sitisho la haraka la mapigano” nchini DRC ifikapo saa kumi na mbili jioni (1600 GMT) Ijumaa, Tete alisema baada ya mazungumzo hayo.

Pande zote pia zilikubaliana kushinikiza “kuondoka mara moja kwa waasi wa M23 kutoka katika maeneo wanayoyakalia”, aliongeza.

Wapiganaji wa kundi la waasi wa M23 wakiondoka kutoka mji wa Sake, kilomita 42 (maili 26) magharibi ya mji wa Goma, mashariki ya DRC Novemba 30, 2012. fighters rebels / Goma DRC Congo. REUTERS/James Akena
Wapiganaji wa kundi la waasi wa M23 wakiondoka kutoka mji wa Sake, kilomita 42 (maili 26) magharibi ya mji wa Goma, mashariki ya DRC Novemba 30, 2012. fighters rebels / Goma DRC Congo. REUTERS/James Akena

Mapambano hayo yalichochea malumbano ya kidiplomasia, huku DRC ikiishutumu Rwanda kwa kuwasaidia waasi, kitu ambacho nchi jirani yake anakanusha.

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambayo Rwanda ni mwanachama, pia imeahidi kupeleka jeshi la pamoja kuzima ghasia hizo.

Wanajeshi wa Kenya waliwasili DRC mapema mwezi huu na Uganda inasema muda si mrefu itapeleka takriban wanajeshi 1,000.

Mwenyekiti wa EAC, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, na Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta -- msimamizi wa EAC anayefanya juhudi za kurejesha amani na usalama katika eneo lililo na utajiri wa madini – walikuwa pia mjini Luanda kuhudhuria mazungumzo hayo.

Rais wa Rwanda Paul Kagame hakuhudhuria mazungumzo hayo kwa udhuru ambao haukufahamika mara moja.

Kabla ya mazungumzo haya, wajumbe wa Baraza la Usalama la UN walitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, wakiwataka waasi wa M23 kuondoka maeneo wanayoyashikilia na kutopatiwa kwa misaada yote ya kigeni kwa waasi wenye silaha ambao siyo serikali , ikiwemo M23.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG