Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:31

Uhuru atembelea Goma wakati wapiganaji wa M23 wajaribu kuuteka mji wa Kibamba


Kenyatta atembelea Goma wakati mapigano yakiendelea karibu na mji huo wa mashariki ya Congo
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:55 0:00

Uhuru Kenyatta awasili Goma kwa ziara ya kujaribu kuziia mapigano kati ya M23 na jeshi la FARDC

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta alitembelea mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wapiganaji wa kundi la M23 walikuwa wanapigana jeshi la taifa FARDC, kaskazini mwa mji huo.

Maafisa wa usalama na wakazi wa mji wa Kibumba wanasema wapiganaji wa M23 wameuzunguka mji huo uliopo kilomita 20 kaskazini mwa Goma wakipambana vikali na wanajeshi wa FARDC.

Kufikia mchana wa Jumanne uvumi ulienea kwamba wapiganaji wa M23 wanakaribia kuuteka kabisa mji huo na kusababisha wimbi jipya la watu kukimbia kuelekea kambi ya watu waliokoseshwa makazi ya Kanyaruchinya, kusini mwa Kibumba.

Hivi karibuni wapiganaji wa M23 walichukua udhibiti wa baadhi ya maeneo ya Kivu Kaskazini , na kuwalazimisha maelfu ya wakazi kukimbia mapigano.

Wakazi wa mashariki ya Kongo wakimbia mapigano mepya wakitokea Kanyaruchinya kuelekea Goma katika jimbo la Kivu kaskazini
Wakazi wa mashariki ya Kongo wakimbia mapigano mepya wakitokea Kanyaruchinya kuelekea Goma katika jimbo la Kivu kaskazini

Kibumba inachukuliwa moja kati ya vizingiti vya mwisho kabla ya waasi kufika Goma, mji wenye karibu watu milioni moja kwenye mpaka na Rwanda.

Afisa mmoja wa usalama asiyetaka kutajwa anasema watu walianza kukimbia baada ya kuwaona wanajeshi wenyewe wakirudi nyuma kuelekea Goma baada ya kupambana vikali na M23.

Gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini Jenerali Constant Ndima akizungumza na waandishi habari amewasihi wakazi kuwa watulivu akisema, "nina taka kuwahakikishia kwamba wanajeshi watiifu wanawazuia maadui kwenye mipaka ya Kibumba."

Mpatanishi wa Jumuia ya Afrika Mashariki EAC, rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, alikua katika kambi ya Kanyaruchinya, wakati uvumi wa wapiganaji kusonga mbele ulikua unaenea.

Aliwaambia waandishi wa habari kwamba amesikia hadithi za "kuvunja moyo."

"Siwezi kupuuza kile nilichokishuhudia." alisema Kenyatta. "Ni lazima niwaambie wote wanaohusika kwamba amuuwezi kujadiliana mnapokabiliwa na janga la kibinadamu."

Ziara ya huko DRC ni hatua ya karibuni katika mfululizo wa juhudi za kupunguza mzozo katika jimbo la mashariki mwa nchi hiyo.

Rais huyo wa zamani aliwasili katika mji mkuu wa Congo wa Kinshasa siku ya Jumapili kwa mazungumzo na wakuu wa serikali kufuatia ziara ya rais wa Angola Joao Lourenco.

Jumuia ya Afrikia Mashariki pia imeitisha mkutano wa amani katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi hapo Novemba 21.

XS
SM
MD
LG