Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Collymore atakumbukwa kwa jitihada kubwa alizofanya kuibadili kampuni ya Safaricom kuwa kampuni kubwa ya mawasiliano Afrika Mashariki yenye thamani ya dola bilioni moja.
Alichukuwa uongozi wa kampuni hiyo mwaka 2010 na kusimamia ongezeko la hisa la takriban asilimia 500, shukran kwa huduma maarufu ya kutuma na kupokea pesa maarufu kama M-Pesa na kuongeza idadi kubwa ya wateja, imesema taarifa hiyo.
Collymore alikuwa na umri wa miaka 61, mwezi May 2019, alikubali kuongoza kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja katika wadhifa huo baada ya serikali ya Kenya kumiliki takriban asilimai 35 ya hisa za kampuni, lakini alisisitiza atafutwe mkenya kuongoza kampuni hiyo.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC