Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 09:03

AFCON 2019 MISRI : Nigeria, Algeria, Misri zaingia raundi ya pili


Mechi kati ya Ivory Coast na Afrika Kusini : Goli la Ivory Coast lililofungwa na Jonathan la kufunguwa dimba kwenye uwanja wa Al Salam, Cairo, Misri Juni 24, 2019. (AP Photo/Hassan Ammar)
Mechi kati ya Ivory Coast na Afrika Kusini : Goli la Ivory Coast lililofungwa na Jonathan la kufunguwa dimba kwenye uwanja wa Al Salam, Cairo, Misri Juni 24, 2019. (AP Photo/Hassan Ammar)

Ni wiki moja sasa imeshapita tangu mechi za makundi husika katika michuano hii ya kulitafuta taifa bingwa barani Afrika ilipoanza, Nigeria, Algeria na Misri zimevuka kuingia raundi ya pili.

Mpaka tunamaliza juma la kwanza la michuano hii timu zilizotolewa ni pamoja na Burundi, Tanzania, Namibia na DRC. Mechi ya kwanza iliyofunguwa michuano hiyo ilichezwa Juni 21, kati ya wenyeji timu ya taifa ya Misri na Zimbabwe katika uwanja wa soka wa kimataifa Jijini Cairo.

Kundi A na B

Timu hizo zikiwa katika mpangilio wa kundi “A” mpaka mwisho wa mchezo, Misri ilikuwa mshindi kwa bao 1 – 0 dhidi ya Zimbambwe. Jumamosi iliyofuata Juni 22 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Uganda zilipambana kwenye kundi A na katika mchuano huo hatimaye Uganda iliibuka kidedea kwa mabao 2 – 0.

Na huko Alexandria kwenye kundi “B”, Juni 22 timu ya Nigeria “Super Eagles” iliibuka mshindi katika mchuano mkali kwa kuifunga Burundi bao 1 – 0. Na kabla siku haijaisha Guinea na Madagascar zikatoka sare ya bao 2 – 2 mjini Alexandria.

Kundi C na D

Na katika uwanja wa Al-Salaam, lilipo kundi “D” Jijini Cairo, Morocco tayari imeshajiwekea matumaini ya kusonga mbele, kwa kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya Namibia, Jumapili iliyopita ya Juni 23.

Senegal ambayo iko kwenye kundi “C” siku hiyo pia ilijiwekea matumaini ya kusonga mbele katika mashindano haya kwa kuicharaza Tanzania bao 2 – 0 katika dimba la Juni 30 ndani ya jiji la Cairo, ambapo baadae kidogo Algeria ikaitandika Kenya 2 – 0 katika dimba hilo hilo.

Na katika kundi “D” nako dunia ilishuhudia Ivory Coast ikiibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya Afrika ya Kusini, Jumatatu ya Juni 24 katika dimba la Al-Salaam jijini Cairo. Siku hiyo hiyo timu za kundi “E” Tunisia na Angola zilitoka sare ya 1 – 1 katika uwanja wa New Suez, huku Mali ikiicharaza Mauritania 4 – 1 katika dimba hilo hilo la New Suez.

Kundi E na F

Na katika kundi “F” Cameroon ikaibuka mshindi wa bao 2 – 0 dhidi ya Guinea-Bissau katika uwanja wa soka wa Ismailia, siku iliyofuata Juni 25, Ghana nayo ikatoka sare na timu ya Benin kwa magoli 2 – 2 katika viwanja hivyo hivyo vya mkoa wa Ismailia.

Tukirejea katika kundi “B” Juni 26, Nigeria iliilaza Guinea bao 1 – 0 katika dimba la Alexandria, huku timu za kundi “A” Uganda na Zimbabwe zikitoka sare ya bao 1 – 1 ndani ya kiwanja cha soka cha kimataifa cha Cairo, ambapo katika kundi hilo hilo Misri nayo ikaitandika DR Congo 2 -0 jijini Cairo.

Tukirudi kwenye kundi “B” tunaikuta Madagascar ikiirejesha nyumbani timu ya taifa ya Burundi baada ya kuicharaza bao 1 – 0 katika mchezo uliochezwa huko Alexandria Juni 26 , ambapo pia katika kundi “C” Algeria ikaibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya Senegal katika mchezo wao ndani ya dimba la Juni 30 na kabla siku hiyo haijakwisha Kenya ikaibuka mshindi wa mabao 3 – 2 dhidi ya Tanzania.

Na hatimaye mpaka ilipofika Juni 29, wiki nzima ikikamilika tunakuta timu za kundi “E” katika dimba la New Suez, zikitoka sare ya goli 1 -1 kati ya Mali na Tunisia, huku kundi “D” Morocco ikiibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya Ivory Coast katika uwanja wa Al-Salaam.

Imetayarishwa na mwandishi wa VOA, Cairo, Misri

XS
SM
MD
LG