Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:48

Harris aitaka jumuiya ya kimataifa kuishinikiza China kuacha uonevu


Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akutana na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh, Hanoi, Vietnam, Agosti, 25, 2021. REUTERS/Evelyn Hockstein/Pool
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akutana na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh, Hanoi, Vietnam, Agosti, 25, 2021. REUTERS/Evelyn Hockstein/Pool

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amesema Jumatano jumuiya ya kimataifa inahitaji kuongeza shinikizo kwa China, dhidi ya madai yake ya eneo juu ya bahari ya kusini mwa China. 

Harris ametoa maelezo yake katika siku yake ya kwanza kwenye mji mkuu wa Vietnam – Hanoi, kabla ya mkutano wa pande mbili na Rais Nguyen Phuc.

Amesema jumuiya ya kimataifa inahitaji kupinga madai ya uonevu ya China na madai mengine ya baharini.

Matumizi ya Harris ya neno “ uonevu” yanajengwa kutokana na shutuma zilizotolewa wakati wa ziara yake ya Singapore Jumatatu kwamba China inaendelea kulazimisha, kutishia na kutoa madai ya kumiliki eneo kubwa la bahari ya kusini mwa China.

Mapema Haris alifanya mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Vietnam, Phan Chinh huko Hanoi ambako baadae aliweka shada la maua katika ziwa Truc bach kumkumbuka John McCain katika maadhimisho ya tatu tangu kifo chake.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris (kushoto) akizungumza na Makamu wa Rais wa Vietnam Vo Thi Anh Xuan katika Ikulu ya Rais, huko Hanoi, Agosti 25, 2021.
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris (kushoto) akizungumza na Makamu wa Rais wa Vietnam Vo Thi Anh Xuan katika Ikulu ya Rais, huko Hanoi, Agosti 25, 2021.

Rubani wa zamani wa jeshi la wanamaji la Marekani alikuwa mfungwa wa vita na baadae akiwa Seneta wa Marekani alisaidia sana kuwaleta pamoja maadui wa kivita.

“Shujaa wa pekee wa Marekani, niliheshimiwa na kupewa nafasi ya kutumika pamoja naye kwa muda mfupi katika Baraza la Seneti la Marekani. John Mccain aliipenda nchi yetu, alikuwa na ujasiri na aliishi maisha ya kishujaa. Kujitoa kwake kulikuwa katika kila kiwango kilichofikiriwa, alipenda nchi yetu na kwa kweli alipigania hadi kufikia hapa sisi ni nani. Na inageuka leo ni kumbukumbu ya kifo chake, kwa hivyo tuko hapo,” Makamu wa Rais alieleza.

Harris pia alitangaza Marekani itatoa dozi nyingine za chanjo ya COVID-19 milioni moja kwa ajili ya Vietnam na alifungua kituo kingine cha Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) huko Hanoi. Ni Makamu wa Rais wa kwanza wa Marekani kutembelea Vietnam.

XS
SM
MD
LG