Biden wakati akiandamana na mwanasheria mkuu Merrick Garland alifanya kikao hicho kutokana na kuwa suala hilo limekuwa tatizo hapa Marekani katika miaka ya karibuni. Takwimu zinaonyesha kuwa vifo kutokana na utumizi wa silaha vitaongezeka pakubwa mwaka huu, ikiwa idadi ya juu zaidi katika kipindi cha miongo miwili.
Tayari mwaka huu, zaidi ya watu elfu 10,700 wameuwawa kwa kupigwa risasi, kulingana na takwimu za kituo kinachofuatilia uhalifu wa matumuzi ya bunduki, baadhi waliuwawa kwa bahati mbaya, lakini wengi waliuwawa katika mauaji ya kukusudiaa, ujambazi na katika mashambulizi ya silaha ya kulenga watu wengi, yaliyoripotiwa zaidi na vyombo vya habari kwenye maeneo mengi hapa Marekani.
Biden ameutaja uhalifu wa matumizi holela ya silaha kuwa janga na tatizo la kimataifa. Mmoja ya hatua zilizochukuliwa na bunge la Marekani ni kusahihisha mapungufu kwenye sheria za kumiliki silaha, kwa kufanya ukaguzi zaidi kwa watu wanaonunua silaha mtandaoni, kwenye maonyesho ya mauzo ya silaha na kwenye akaunti za benki za watu binafsi.
Hatua nyingine, ni kuwapa maafisa siku 10 za kazi badala ya siku 3 ili waweze kufanya ukaguzi kwa watu wanaonunua silaha. Lakini baraza la Seneti ambalo limegawanyika nusu kwa nusu bado halijachukua hatua yoyote, na haiko wazi iwapo Wademocrats wenyewe watajiunga na makamu rais Kamala Harris katika upigaji kura, ili kupata za kutosha.