Hatua hiyo imechukuliwa ili kukabiliana na virusi vya Corona kwenye mji huo wenye wakaazi milioni tano.
Mamlaka bado inataabika kuzuia ongezeko la mlipuko wa aina mpya ya virusi vya Delta vya COVID-19.
Kufungwa kwa shughuli za umma hivi karibuni nchini humo kulitangazwa Juni 26, baada ya dereva wa gari aina ya Limousine, kwenye uwanja wa ndege wa Sydney, ambaye alikuwa akisafirisha wafanyakazi wa anga wa kimataifa, alipopimwa na kukutwa ana maambukizi ya aina mpya ya virusi.
Zaidi ya watu 300 wameambukizwa tangu wakati huo. Mlipuko umeongezeka kufikia hadi watu zaidi ya 300 pamoja na kesi mpya 27 zilizoripotiwa Jumatano.
Australia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuzuia kusambaa kwa COVID-19 kutokana na juhudi kali za kufunga shughuli za umma.
Mpaka sasa nchi hiyo imetangaza jumla ya kesi 30,861 pekee zilizothibitishwa na vifo 910, kulingana na kituo kinachofuatilia kesi za virusi vya Corona cha John Hopkins cha Marekani.