Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:07

Idadi ya watazamaji katika ufunguzi wa Olimpiki Tokyo itapunguzwa kwa watu wachache


Watu wakizungumza karibu na mnara wa Ollimpiki nje ya ofisi za Kamati ya Olimpiki ya Japani (JOC)
Watu wakizungumza karibu na mnara wa Ollimpiki nje ya ofisi za Kamati ya Olimpiki ya Japani (JOC)

Waandaaji wa Olimpiki walitangaza watawaruhusu watu 10,000 tu au asilimia 50 ya uwezo wa ukumbi kuingiza watu katika hafla zote

Idadi ya watazamaji katika hafla ya ufunguzi wa Olimpiki ya Tokyo itapunguzwa kwa watu wachache Viongozi muhimu sana, na maafisa wa Olimpiki kwa sababu ya wasiwasi juu ya kuongezeka kwa kesi mpya za COVID-19 katika mji mkuu kulingana na Gazeti moja la Kijapani.

Ripoti katika toleo la Jumanne la gazeti la Asahi Shimbun inasema wazo hilo ni sehemu ya mpango mkubwa ambao utajumuisha pia kupiga marufuku wageni kuhudhuria hafla katika kumbi kubwa pamoja na saa za usiku.

Waandaaji wa Olimpiki ya Tokyo walitangaza Juni 21 kwamba itawaruhusu watu 10,000 tu, au asilimia 50 ya uwezo wa ukumbi kuingiza watu katika hafla zote, licha ya wataalam wa afya kuishauri serikali kwamba kupiga marufuku watazamaji wote ilikuwa chaguo lenye hatari ndogo zaidi katika michezo yote.

Asahi Shimbun iliripoti mabadiliko yaliyopitiwa kwa idadi ya watazamaji walioruhusiwa itajadiliwa kati ya serikali na maafisa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki.

XS
SM
MD
LG