Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:13

Maambukizi ya COVID-19 yavunja rekodi Afrika Kusini


Mwili wa mtu aliyefariki kutokana na corona wakekwa kwenye gari Afrika kusini katika picha ya awali
Mwili wa mtu aliyefariki kutokana na corona wakekwa kwenye gari Afrika kusini katika picha ya awali

Maafisa wa afya wa Afrika kusini wamesema Jumapili kwamba wimbi jipya la virusi vya corona nchini humo limevunja rekodi kwenye maambukizi ya kila siku.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP zaidi ya kesi 26,000 mpya ziliripotiwa Jumamosi ikilinganishwa na 24,000 zilizoripotiwa Ijumaa kulingana na idara ya kitaifa ya magonjwa ya kuambukizwa.

Maambukizi ya sasa yanesemekana kuwa ya juu zaidi Afrika Kusini tangu janga la corona lilipoingia nchini humo. Ripoti zinasema kuwa tayari kuna wagonjwa zaidi ya 13,800 wa covid kwenye hospitali za Afrika kusini ikisemekana kuwa baadhi ya hospitali zinaahirisha baadhi ya upasuaji ili kuweza kuhudumia wagonjwa hao.

Vifo kutokana na corona nchini humo vimefika zaidi ya 63,000 ingawa baadhi ya takwimu kuhusu idadi ya vifo huenda ikawa zaidi ya 170,000. Kesi milioni 2 za covid Afrika kusini ni zaidi ya asilimia 30 ya jumla ya kesi zote zilizoripotiwa barani Afrika kulingana na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa.

XS
SM
MD
LG