Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:19

Afrika Kusini : Maafisa waripoti vifo na ongezeko la COVID-19

Wafanyakazi wa afya wakivalia vifaa vya kujilinda na maambukizi ya COVID-19 (PPE) wakijitayarisha kumpima mwanamke iwapo ana maambukizi ya COVID-19 katika hospitali ya Fourways Life Johannesburg, Juni 28, 2021. Photo by Emmanuel Croset / AFP)

Maafisa wa Afrika Kusini wanasema nchi inakabiliwa na ongezeko la maambukizo ya ugonjwa wa COVID-19, wakisema kumekuwepo na watu 15,000 walioambukizwa Jumapili na watu 122 wamefariki.

Rais Cyril Ramaphosa alisema Jumapili usiku kuwa aina ya virusi vya corona, Delta inawezekana ndio inayosambaa na kusababisha kuongezeka kwa haraka wagonjwa nchini humo.

Masharti mapya kupambana na mlipuko huo ni pamoja na kupiga marufuku mikusanyiko yote ya umma isipokuwa mazishi, ambayo yatapunguzwa kwa watu 50 tu. Uuzaji wa pombe pia utakatazwa na muda wa kutotoka nje wa usiku utaanza kutumika.

Jimbo la Gauteng lilikuwa na asilimia 66 ya maambukizi mapya, maafisa walisema.

Mafisa wa afya wana wasiwasi majimbo mengine hivi karibuni huenda yakapata ongezeko la wagonjwa.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG