Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:08

Marekani huwenda isitimize asilimia 70 ya watu kupatiwa chanjo ifikapo Julai nne


Mfano wa sehemu zinazotoa chanjo bure dhidi ya COVID-19 nchini Marekani
Mfano wa sehemu zinazotoa chanjo bure dhidi ya COVID-19 nchini Marekani

White House imesema juhudi mpya zinafanywa kuwapatia chanjo watu wazima katika umri wa miaka 18 hadi 26 ambao kwa sababu mbali mbali wameonyesha hamasa kidogo katika kupatiwa chanjo tangu idadi ya kesi mpya za virusi vya Corona pamoja na vifo kupungua haraka katika wiki za karibuni

Marekani itashindwa kufikia lengo la Rais Joe Biden la kuwapatia chanjo takriban asilimia 70 ya watu wazima Marekani kwa angalau dozi moja au kamili dhidi ya virusi vya Corona ifikapo siku ya uhuru hapo Julai nne, lakini White House inasema inatarajia kufikia kiwango hicho katika wiki chache zijazo.

Katika tathmini mpya Jumanne juu ya juhudi za chanjo nchini Marekani mratibu wa majibu ya COVID-19, Jeff Zients, alisema serikali kuu inatarajia kwamba asilimia 70 ya watu wenye miaka 27 na zaidi watakuwa wamepata angalau dozi moja ya chanjo ifikapo Julai nne, ambapo alielezea kama mafanikio makubwa.

Tunaingia msimu wa majira ya joto kali tukiwa na furaha, majira ya joto yaliyo huru.

Hivi sasa amesema juhudi mpya zinafanywa kuwapatia chanjo watu wazima, katika umri wa miaka 18 hadi 26 ambao kwa sababu mbali mbali wameonyesha hamasa kidogo katika kupatiwa chanjo hususan tangu idadi ya kesi mpya za virusi vya Corona pamoja na vifo kupungua haraka katika wiki za karibuni hapa nchini, na biashara kufunguliwa tena bila masharti ya watu kuvaa barakoa na kutokaribiana kutoka mtu hadi mtu, suala ambalo lilikuwa likitekelezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Mfano wa chanjo dhidi ya COVID-19
Mfano wa chanjo dhidi ya COVID-19

Juhudi zetu haziishii Julai nne, Zients alisema. Ni muhimu sana kuliko hapo awali kwamba wanapata chanjo, pamoja na wengine ambao bado hawajachoma chanjo dhidi ya COVID-19. Virusi vya Corona vinasababisha ugonjwa wa COVID-19.

Dr. Rochelle Walensky, mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) Marekani alisema tunashuhudia kupungua kwa kasi vifo na wagonjwa kulazwa hospitalini. Alisema kuwa ni mafanikio yaliyothibitishwa na chanjo zilizopo, ikiwemo dhidi ya aina ya virusi vya Corona asilia, kwa hivi sasa kila kifo cha COVID kinaweza kuzuilika kabisa.

XS
SM
MD
LG