Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:17

Tanzania yakabiliwa na wimbi la tatu la COVID-19


Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema Ijumaa wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona limeikumba taifa na kwamba wagonjwa wa COVID-19 wapo.

Rais amewaomba viongozi wa dini kuwakumbusha waumini kuhusu umuhimu wa kujikinga na ugonjwa huo, ili taifa liweze kujiepusha na vifo vya makundi makundi.

Samia amezungumza hayo mkoani Dar es Salaam, alipokutana na viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini (TEC).

Rais ametumia nafasi hiyo pia kuwaomba viongozi wa dini nchini kutoa elimu ya kujikinga kwa waumini wao, ikiwemo kusisitiza wachukue tahadhari na kufuata ushauri unaotolewa na wataalam wa afya.

“Sasa hivi kuna wimbi la tatu la Corona, ishara ndani ya nchi tayari zinaonekana tuna wagonjwa ambao wameshaonekana katika hili wimbi la tatu, kama mnakumbuka siku nimetembelea hospitali ya Mwananyamala daktari aliniambia kuna wodi ya wagonjwa wenye matatizo ya kupumua,” alisema Rais Samia.

Rais Samia ameongeza : ”Daktari nikamuambia ni COVID-19 akasema ndiyo, wakati wapiga picha wangu walikuwa wamekwisha tangulia nikawaambia nyinyi hebu tokeni haraka huko, hili jambo lipo, tunawaomba sana viongozi wa dini mlisemee hili kwa waumini ili tujiepushe na vifo vya makundi”.

Vyanzo vya Habari Tanzania

XS
SM
MD
LG