Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:04

'Wajapani wengi bado wanapinga Olimpiki kufanyika'

Mandhari ya uwanja wa taifa (katikati), eneo kuu ambapo itafanyika michezo ya Olimpiki 2020, Tokyo, Juni 21, 2021. (Photo by Kazuhiro NOGI / AFP)
Mandhari ya uwanja wa taifa (katikati), eneo kuu ambapo itafanyika michezo ya Olimpiki 2020, Tokyo, Juni 21, 2021. (Photo by Kazuhiro NOGI / AFP)

Uchunguzi wa maoni kwa miezi kadhaa ulionyesha Wajapani wengi wanapinga kufanyika kwa michezo ya Olimpiki.

Baadhi ya wataalam wa afya wameonya kwamba hafla hiyo inaweza kusababisha milipuko ya corona au kusambaa kwa aina mpya ya virusi.

Lakini ikiwa imesalia mwezi mmoja tu hadi kuwasha mwenge wa Olimpiki huko Tokyo, waandaaji wanaamini kwamba wanaweza kufanikisha michezo hiyo kwa salama, shukran kwa kiasi fulani kwa tahadhari kwa janga hilo ambapo utahakikisha kuwa michuano ya Olimpiki ya msimu wa joto ni ya kipekee kuliko mingine yeyote katika historia.

Watazamaji wa kimataifa tayari wamepigwa marufuku katika michuano hiyo ambayo inaanza Julai 23. Jumatatu.

Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga akiwa katika mkutano na waandishi wa habari.
Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga akiwa katika mkutano na waandishi wa habari.

Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga alisema ni dhahiri inawezekana mashindano hayo yakafanyika katika viwanja vitupu kabisa, kulingana na hali ya COVID-19 nchini Japan.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG