Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetoa onyo la kiwango cha nne ambacho ni kikubwa zaidi ikisema ni kutokana na kasi ndogo ya utoaji chanjo nchini Japan, pamoja na masharti makali dhidi ya raiya wake wanao kusudia kuhudhuria michezo hiyo.
Onyo tofauti pia limetolewa na idara ya kudhibiti na kuzuia mogonjwa kuenezwa ya Marekani CDC, ikishauri hata wale walio pokea chanjo dhidi ya kuzuru Japan kutokana na hatari ya kuambukizwa au kueneza aina tofauti ya virusi vya corona.
Michezo ya Olimpiki imepangwa kuanza Julai 23 hadi Agosti 8, baada ya kuahirishwa mwaka uliyopita kutokana na janga hilo. Tokyo pamoja na miji kadhaa iko chini ya uangalizi wa dharura ili kudhibiti wimbi jipya la maambukizi ambayo yameelemea mahospitali kote nchini, wakati wito wa kuahirisha michezo hiyo ukiendelea kuongezeka.
Mtayarishaji- Harrison Kamau