Biden atatembelea eneo la Rzesow, lililo umbali wa kilometa 50 kutoka mpakani mwa Ukraine, ambako anatarajiwa kukutana na Rais wa Poland, Andrzej Duda.
Ni sehemu ya safari yake ya dharura barani Ulaya ambayo imesababiswha na vita vya Ukraine, ambapo pia ameshiriki mikutano kasha nchi Ubelgiji.
Akiwa nchini Poland, Bidenpia atapokea taarifa ya namna gani nchi hiyo inakabiliana na wimbi la mamilioni ya wakimbizi, ambao wanakimbia makombora ya Russia nchini Ukraine.
Rais huyo pia atakutana na wanajeshi wa kikosi cha anga ambao wana kambi yao katika eneo hilo la Rzeszw.
Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya umeishutumu Russia, kwa kile ulichokiita “uhalifu wa kivita chini Ukraine.”
Azimio la viongozi wa Umoja huo, baada ya mkutano wao mkuu mjini Brussels, Ubelgiji, linasema serikali ya Russia itawajibishwa, kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Baraza la Ulaya limesema kuwa Russia imekuwa ikitekeleza mashambulizi dhidi ya umma, na kuyalenga maeneo ya watu, ikiwa ni Pamoja na hospitali, viwanda vya dawa, shule na makazi.