Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:48

Biden kuhudhuria mkutano wa NATO Ubelgiji


Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden.

Rais wa Marekani Joe Biden anasafiri Jumatano kuelekea Brussels, Ubelgiji, ambako atakutana na viongozi wa muungano wa kijeshi wa NATO na washirika wa Ulaya, ambapo anatarajiwa kutangaza duru mpya ya vikwazo dhidi ya Russia kwa uvamizi wake dnchini Ukraine.

Msahuri wa usalama wa kitaifa wa White House Jake Sullivan alwaambia waandishi wa habari: "Ataungana na washirika wetu katika kuweka vikwazo zaidi kwa Russia na kuimarisha vikwazo vilivyopo ili kukabiliana na ukwepaji na kuhakikisha utekelezwaji thabiti."

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy anatarajiwa kuhutubia – kwa njia ya video - mkutano mkuu wa NATO siku ya Alhamisi, na alisema kabla ya mkutano huo kwamba anatarajia viongozi wa nchi za Magharibi kuongeza vikwazo vyao dhidi ya Russia na kuahidi msaada zaidi kwa Ukraine.

Takriban mwezi mmoja baada ya vikosi vya Russia kuivamia Ukraine, kuna ishara zinazoongezeka kwamba vikosi vya Ukraine vina ujasiri mkubwa, vikilenga wanajeshi wa Russia na, wakati mwingine, kuchukua udhibiti wa maeneo yaliyokuwa yametwaliwa na Russia,

Wizara ya Ulinzi ya Ukraine ilisema Jumanne kwamba vikosi vyake vimechukua tena Makariv, kitongoji cha mji mkuu wa Kyiv, kufuatia mapigano makali.

Wanajeshi wa Ukraine pia walionekana kuanzisha mashambulizi katika mji wa mashariki wa Izyum, kilomita 120 kusini mashariki mwa Kharkiv, na katika maeneo ya karibu na mji wa Kherson, kusini mwa nchi hiyo.

Akitoka Ubeklgiji, Biden anatarajiwa kufanya ziara nchini Poland.

XS
SM
MD
LG