Ukraine ilikataa mapendekezo ya Russia kuusalimisha mji uliozingirwa wa Mariupol siku ya Jumatatu huku vikosi vya Russia vikiendeleza mashambulizi zaidi katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.
Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine, Irina Vereshchuk alikataa ombi la Russia na kusema Russia inapaswa kufungua njia za kibinadamu ili watu waweze kuondoka Mariupol. Hayawezi kuwepo mazungumzo yoyote ya kujisalimisha au kuweka silaha chini. Tayari tumeuarifu upande wa Russia kuhusu hili Vereshchuk alikiambia chombo cha habari cha Ukraine, Pravda.
Kulingana na shirika la habari la serikali la Russia (RIA), wizara ya ulinzi ya Russia iliwapa wanajeshi wa Ukraine hadi alfajiri ya Jumatatu na kwamba wakikataa kujisalimishakama itakuwa wanashirikiana na majambazi.
Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alielezea hatua za Russia huko Mariupol kuwa ni mbaya.