Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:03

Viongozi wa G7 waanza mkutano 'maalum' Brussels


Viongozi wa NATO waanza mkutano mkuu mjini Brussels, Ubelgiji, kujadili mikakati ya ziada ya kukabiliana na uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine.
Viongozi wa NATO waanza mkutano mkuu mjini Brussels, Ubelgiji, kujadili mikakati ya ziada ya kukabiliana na uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine.

Viongozi wa nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani G7, ambazo pia ni wanachama wa muungano wa kijeshi wa NATO, wanakutana Alhamisi mjini Brussels, Ubelgiji,  kujadili mikakati ya muda mfupi na ile ya muda mrefu, ya kukabiliana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Kabla ya mkutano huo, rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alituma ujumbe kwa njia ya video, kwa lugha ya Kiingereza, kuwasihi wanachama wa NATO kuipatia Ukraine msaada zaidi "wenye ufanisi na usio na vikwazo", ikiwa ni pamoja na silaha kwa vikosi vyake.

Zelenskyy pia alitoa wito kwa watu kote ulimwenguni kufanya maandamano dhidi ya Russia kwa kuivamia Ukraine.

Mbali na mazungumzo ya NATO, Rais wa Marekani Joe Biden anakutana na viongozi wa G-7 na Baraza la Ulaya.

Mshauri wa usalama wa taifa Jake Sullivan alisema lengo kuu ni kuona kwamba "umoja na ushirikiano, ambao tumeona kwa mwezi uliopita utadumu kwa muda mrefu iwezekanavyo."

Sullivan alisema hiyo inajumuisha nchi zinazotimiza ahadi za kutoa vifaa vya kijeshi kwa Ukraine, kutekeleza vikwazo vilivyopo dhidi ya Russia, na kutafuta njia za kuongeza misaada ya kibinadamu, kwa wale walioathiriwa na mashambulizi hayo.

Biden anatarajiwa kutangaza duru mpya ya vikwazo vinavyowalenga wanasiasa wa Russia, matajiri wenye ushawishi mkubwa, na watu wengine. Baadaye ataelekea nchini Poland kwa mazungumzo zaidi.

XS
SM
MD
LG