Maoni yamekuja wakati Lukashenko akiwa mwenyeji wa Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu.
Kulingana na BelTA, Lukashenko alieleza mazungumzo yake na Rais wa Russia Vladimir Putin wiki iliyopita, na kusema viongozi hao wawili walijadili umuhimu wa Russia kuilinda Belarus “ kama eneo lake binafsi” iwapo kutakuwa na uchokozi unaoelekezwa Belarus.
Putin alielemewa na ukosoaji mwezi uliopita alipotangaza kuwa Russia itapeleka silaha za nyuklia za mbinu ya hali ya juu huko Belarus.
Majeshi ya Russia pia yameitumia Belarus kama ni eneo la kuanzisha uvamizi kamili huko Ukraine zaidi ya mwaka moja uliopita, baada ya washirika wawili kusisitiza walikuwa wanafanya mazoezi ya kijeshi tu na hawakuwa na mpango wa kuishambulia Ukraine.
Mikoa miwili ya Ukraine – Kharkiv upande wa kaskazini mashariki na Zaporizhzhia huko kusini mashariki – zimeshambuliwa na makombora, roketi na mizinga ya Russia wakati wa wikiendi, jeshi la Ukraine limeripoti Jumapili.
Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari yahe Associated Press, Agence France-Presse na Reuters.