Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:36

Belarus yaitaka Russia kuihakikishia usalama


Rais wa Belarus Alexander Lukashenko akutana na waziri wa ulinzi Sergei Shoigu mjini Minsk.
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko akutana na waziri wa ulinzi Sergei Shoigu mjini Minsk.

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, amesema leo Jumatatu kwamba nchi yake inahitaji hakikisho la usalama kutoka kwa Russia, kulingana na shirika la utangazaji la BelTA.

Lukashenko ametoa kauli hiyo, wakati akimkaribisha Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu.

Kulingana na BelTA, Lukassenko alitaja mazungumzo yake na Rais wa Russia Vladimir Putin wiki iliyopita, akisema kwamba walijadili haja ya Russia kulinda Belarus "kama eneo lake," ikiwa kungekuwa na "uchokozi" dhidi ya nchi hiyo.

Putin alikosolewa mwezi uliopita, alipotangaza kwamba Russia ingepeleka silaha za kinyuklia nchini Belarus.

Vikosi vya Russia pia vilitumia Belarus kama eneo la kuanzisha uvamizi kamili wa Ukraine, zaidi ya mwaka mmoja uliopita, baada ya washirika hao wawili kusisitiza kwamba walikuwa wakifanya mazoezi ya kijeshi tu, bila mpango wowote wa kuishambulia Ukraine.

Mikoa miwili ya Ukraine - Kharkiv iliyo kaskazini-mashariki, na Zaporizhzhia kusini-mashariki - ilipigwa na makombora ya Russia, mwishoni mwa juma, jeshi la Ukraine liliripoti Jumapili.

XS
SM
MD
LG