“Huu ni mjadala hatari na unatia wasiwasi,” Biden aliwaambia waandishi wa habari huko White House.
Kiongozi wa Russia Jumamosi alitangaza kwamba aliamuru kupelekwa silala za kimbinu za Russia nchini Belarus, ambayo inaongozwa na dikteta mwenzake Alexander Lukashenko mmoja wa washirika wa karibu wa Russia.
Washington ililaani mpango huo, ambao unafuata jaribio la Russia la zaidi ya mwaka mmoja kudhibiti mshirika wa nchi za magharibi, Ukraine ambayo ni jirani wa Russia na Belarus.
Hata hivyo, maafisa wa Marekani hawajaona ishara yoyote kuwa Russia imepeleka zana za nyuklia.
“Bado hawajafanya hilo,” Biden amesema.