Ikiwa siku moja baada ya mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa China kufanya ziara mjini Moscow na kuahidi ushirikiano wa dhati na Russia, Beijing ilijizuia kuonyesha msimamo wake katika kura hiyo, ikiwa ni mara ya nne kuchukua hatua kama hiyo tangu Russia iivamie Ukraine Februari 24 mwaka jana.
Azimio hilo lilipitishwa Alhamisi kwa kura 141 za kuliunga mkono na 32 za wanachama ambao hawakuonyesha msimamo wao.
Nchi sita ziliungana na Russia kwa kupinga azimio hilo. Nazo ni Belarus, Korea Kaskazini, Eritrea, Mali, Nicaragua na Syria.
“Azimio hili ni ishara kubwa ya kuungwa mkono kimataifa kwa Ukraine,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy aliandika ujumbe huo kwenye Twitter baada ya kura hiyo.