Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:39

Wizara ya ulinzi ya Uingereza inaelezea wasiwasi wake kwa Vladimir Kolokoltsev


Waziri wa mambo ya ndani wa Russia, Vladimir Kolokoltsev
Waziri wa mambo ya ndani wa Russia, Vladimir Kolokoltsev

Kiuhalisia wizara ya mambo ya ndani ya Russia ilisema katika taarifa mpya za kijasusi zilizochapishwa kwenye Twitter kwamba sehemu kubwa ya eneo lililobaki bado ni eneo la mapigano lenye fursa chache  za upatikanaji wa huduma za msingi kwa raia wengi

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumapili kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani wa Russia, Vladimir Kolokoltsev kutoa ripoti kuu katika kikao kamili cha karibuni cha Baraza la Usalama la Russia ilikuwa ni jaribio la kurekebisha hali kwenye maeneo ya Ukraine ambayo waliyanyakua kinyume cha sheria.

Kiuhalisia wizara hiyo ilisema katika taarifa mpya za kijasusi zilizochapishwa kwenye Twitter sehemu kubwa ya eneo lililobaki bado ni eneo la mapigano lenye fursa chache za upatikanaji wa huduma za msingi kwa raia wengi.

Baraza la Usalama la Russia lilikutana wiki iliyopita kwa mara ya kwanza tangu Oktoba mwaka 2022. Kufuatia kurejeshwa kwa watoto 31 nchini Ukraine mkuu wa Ofisi ya Rais wa Ukraine, Andriy Yermak, alisisitiza katika mazungumzo ya simu Jumamosi na Amal Clooney mwanasheria maarufu wa haki za binadamu juu ya umuhimu wa kuwarudisha watoto wote waliofukuzwa kwenda nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG