Maria Lvova Belova ambaye ni kamishna wa watoto kwenye ofisi ya rais amesema kwamba “ kwa bahati mbaya hakuna mawasiliano rasmi kupitia mitandao rasmi na Ukraine, ingawa tupo tayari kushirikiana na wahusika wote.” Ameongeza kusema kwamba kufikia sasa hawajapata mwaliko rasmi kando na kupitia kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Lvova Belova amezungumza kwa njia ya video kwa vile hawezi kusafiri kimataifa kwa hofu ya kukamatwa na kupelekwa kwenye mahakama ya ICC mjini the Hague. Tayari hati ya kukamatwa pamoja na Putin ilitolewa na ICC hapo Machi 17.