Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 05:11

Baraza la Utawala la Sudan kukutana na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika


Mwenyekiti wa Tume  ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat akiwa Khartoum, Feb. 5, 2019.
Mwenyekiti wa Tume  ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat akiwa Khartoum, Feb. 5, 2019.

Mkuu wa Baraza la Utawala la Sudan Jenerali Abdel Fattah Burhan amekutana na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat mjini Khartoum Jumapili kujadili masuala ya kisiasa nchini Sudan.

Mtaalamu wa masuala ya uhusiano wa kimataifa wa Sudan, Dr al-Rasheed Ibrahim amesema makubaliano yoyote au juhudi zitasaidia mkakati wa uthabiti wa Afrika.

Dkt Ibrahim ameeleza : "Naamini kuwa kuna makubaliano yaliyofikiwa katika kiwango hiki cha Umoja wa Afrika, na haiwezekani kuiachia Marekani na ziara ya mjumbe wa Marekani katika Pembe ya Afrika kuhusu hili.

Bila shaka, makubaliano yoyote au juhudi zitasaidia mkakati wa uthabiti Afrika na hii itasaidia mjadala ambao ulianzishwa na Bwana Voker Perthes mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuungwa mkono na Baraza Kuu."

Ameendelea kusema : "Lakini vyama vya kisiasa nchini sudan vimezusha swali kwa kusema kuwa hakuna mazungumzo , hakuna ushirikiano, utawaweka katika mapambano na jumuiya ya kimataifa na hata pia na mpatanishi wa Afrika."

Faki pia atakutana na vyama vya upinzani kusikiliza na kujadiliana nao kuhusu mtazamo wao katika ziara yake ya siku mbili nchini humo.

Maafisa wa kijeshi wa Sudan wamemkamata tena afisa wa juu wa zamani wa serikali , chama chake kimesema wakati makundi ya kutetea demokrasia Jumatatu yameanza tena maandamano zaidi kupinga mapinduzi ya kijeshi ambayo yametumbukiza nchi katika machafuko.

XS
SM
MD
LG