Vikosi vya usalama vya Sudan vilifyatua gesi ya kutoa machozi Jumatatu kwa maelfu ya waandamanaji wanaotaka utawala wa kiraia na haki kwa waandamanaji waliouawa tangu mapinduzi ya mwaka 2021 mashahidi na mwandishi wa habari wa shirika la AFP walisema.
Gesi ya kutoa machozi ilirushwa wakati waandamanaji waliokuwa wakielekea kwenye makazi ya rais katika mji mkuu Khartoum katika maandamano ya karibuni dhidi ya mapinduzi ya Oktoba 2021 yaliyoongozwa na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan mwandishi huyo alisema.
Waandamanaji walionekana wakirusha mawe kwa vikosi vya polisi huku wengine wakiwasaidia watu waliojeruhiwa kwa gesi ya kutoa machozi mwandishi huyo aliongeza.
Jumatatu waandamanaji wanaopinga mapinduzi katika mji wa Wad Madani kusini mwa Khartoum walionekana wakipeperusha bedera za Sudan na kubeba mabango ya watu waliouawa katika msako huo. Hapana kwa utawala wa kijeshi, na damu kwa damu, walipiga kelele kulingana na mashahidi. Mamia pia walikusanyika katika mji wa bahari ya shamu wa Port Sudan wakaazi wa huko walisema.