Taarifa ya UN imesema mzozo binafsi baina ya wanaume wawili kutoka kabila la Masalit na wahamaji wa Kiarabu wamesababisha ghasia karibu na mji wa El Geneina.
Kundi la Nomad lililokuwa na silaha lilivamia soko la ndani na kuchoma moto sehemu ya kijiji na kuua watu tisa wakiwemo watoto wawili.
Mapigano pia yamesababisha watu 4,000 kukimbilia katika mpaka wa Chad.
Zaidi ya watu milioni mbili bado wanaishi katika kambi kutokana na matokeo ya mzozo wa Darfur katika miaka ya 2000.
Mwaka 2021 umeshuhudia ghasia mpya huko Darfur kukiwa na mashambulizi ya mara kwa mara katika vijiji yanayofanywa na wanamgambo.