Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 04:22

WFP yasitisha operesheni zote za misaada Jimbo la Darfur Kaskazini


Darfur, Sudan
Darfur, Sudan

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesitisha operesheni zake kote nchini Sudan katika jimbo la Darfur Kaskazini kufuatia mashambulizi ya karibuni kwenye ghala zake, uamuzi ambao ulitarajiwa kuwaathiri takriban watu milioni 2 katika eneo hilo.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo la Umoja wa Mataifa ilisema ghala zake zote tatu katika eneo hilo zilishambuliwa na kuibiwa. Zaidi ya tani 5,000 za chakula ziliibiwa, kundi hilo limesema.

Mapema wiki hii, WFP ilisema watu wasiojulikana waliokuwa na silaha walishambulia moja ya ghala zake katika mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini wa El Fasher. Ikijibu hali hiyo, mamlaka ya kieneo iliamua kuweka amri ya kutotoka nje kote katika jimbo hilo.

Hata hivyo, mashambulizi yaliendelea mpaka mapema Alhamisi, taarifa imesema. Mamia ya watu waliofanya wizi katika ghala hiyo pia walilivunja majengo, WFP imesema.

“Wizi huu umewanyima takriban watu milioni mbili chakula na lishe ya kuwasaidia watu wenye shida,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa WFP David Beasley. “Siyo tu ni kuturudisha nyuma sana katika operesheni zetu kote nchini, lakini pia inahatarisha wafanyakazi wetu na kudumaza uwezo wetu wa kukidhi mahitaji ya familia nyingi zilizo katika mazingira hatarishi.”

Idara hiyo imesema haiwezi kubadili misaada kutoka sehemu nyingine katika taifa hilo la Afrika Mashariki na kuzipeleka kwenye ghala zilizoibiwa bila ya kuvuruga kabisa mahitaji ya wananchi wa Sudan ambao wanaishi nje ya jimbo hilo.

Sudan ni moja ya nchi maskini sana duniani, yenye takriban watu milioni 11 wenye shida ya chakula na kuhitaji misaada katika maisha yao mwaka huu wa 2022, imesema WFP.

Shirika hilo limeisihi mamlaka ya Sudan kujaribu kufanikisha kupatikana kwa bidhaa zilizoibiwa na kutoa dhamana ya usalama kwa operesheni za WFP huko Darfur Kaskazini.

Alhamisi, shirika la habari la serikali liliripoti kwamba washukiwa kadhaa walikamatwa huko El Fasher baada ya kuonekana wamepanda kwenye magari na mikokoteni iliyokuwa ikisukumwa na wanyama wakiwa na sherehe ya chakula ambacho kinasadikiwa kiliibiwa kutoka kwenye ghala za WFP. shirika hilo SUNA halikusema watu wangapi wamekamatwa.

Uamuzi wa WFP umekkuja huku kukiwa na mivutano ya kisaisa ambayo ilifuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Oktoba.

Ijumaa, kundi la madaktari lilisema kwamba watu watano wlaiuawa katika maandamano dhidi ya mapinduzi hayo, ambayo yalizuka katika majimbo kadhaa kote nchini. Majeshi ya usalam yalitumai gesi ya kutoa machozi na risasi za moto kuwatawanya maelfu ya waandamanaji, kundi hilo lilisema. Huku maafa ya Alhamisi, yalifikisha idadi ya vifo tangu mapinduzi kupanda hadi watu 53.

Wakati huo huo polisi wa Sudan wamekiri katika taarifa yao Ijumaa kwamba waandamanaji wanne waliuawa na zaidi ya 290 kujeruhiwa katika maandamano. Taarifa ilibandikwa na SUNA lakini haikutaja polisi kutumia gesi ya kutoa machozi au risasi za moto. Polisi waliongeza kwamba zaidi ya polisi 40 walijeruhiwa katika mapambano hayo na waandamanaji.

XS
SM
MD
LG