Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:31

Hofu yatanda baada ya M23 kuteka miji kadhaa mashariki mwa DRC


Mlipuko katika mji wa Kanyabayonga, DRC. Picha na Austere Malivika. Juni 29, 2024
Mlipuko katika mji wa Kanyabayonga, DRC. Picha na Austere Malivika. Juni 29, 2024

Wakazi wa miji mbalimbali katika jimbo la Kivu kaskazini, lililo mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, wameiomba serikali kuu ya Kinshasa kutafuta suluhisho la haraka kumaliza mapigano kati ya wanajeshi wa serikali ya waasi wa M23, ambao wameteka miji kadhaa.

Baadhi ya wakaazi wamebaki chini ya udhibiti wa waasi wa M23 baada ya jeshi tiifu kwa serikali, FARDC, kutimuliwa kutoka kwenye miji ya Kanyabayonga, Kayna, Luofu, Miriki na Kimaka wilayani Lubero, huku wakiishutumu serikali kwa kushindwa kuwalinda dhidi ya uvaamizi wa waasi.

Kasereka Swing mmoja wa viongozi wa mashirika ya kiraia katika katika mji wa Kanyabayonga akiwa uhamishoni katika mji wa Kirumba kwa sasa asema hali ni ya wasiwasi kuhusu usalama wa raia ambao kwa sasa wamebaki katika udhibiti wa M23 baada ya jeshi la serikali kushindwa katika mapigano na kukimbilia mesneo ya Alibongo, Kaseghe, Lubero na wengine katika mji wa Butembo.

"Hali hiyo inzusha wasiwasi mkubwa kwa wanavijiji," alisema Swing.

Tukio hilo linatajwa kama pigo kubwa kwa serikali ya Kinshasa ambayo imepoteza udhibiti wa miji muhimu katika wilaya ya Lubero, iliyo na idadi kubwa zaidi ya watu katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Wakati wa Mapigano hayo, watu nane wamepoteza maisha, watatu katika mji wa Kirumba wengine katika mji wa Kayna, wengi wakiuawa kwa risasi mabomu yaliyokuwa yakirushwa na pande zote husika katika Vita.

Kuchukuliwa kwa miji ya Kanyabayonga, Kayna, Kimaka, Luofu na Kirumba na waasi wa M23 pia ni pigo kubwa uongozi wa mkoa wa Kivu kaskazini unao ongozwa na gavana wa kijeshi.

Pamoja na hayo kwa sasa, mji wa Goma umekuwa katika hali ya wasiwasi kubwa kufatia waasi wa M23 kuendelea kuongeza idadi ya waanamgambo wake kwenye uwanja wa mapigano.

Vita mashariki mwa Congo vimepelekea maelfu ya watu kuhama makaazi yao na kuwa wakimbizi wa ndani.

M23 kwa sasa inaonekana kuwa na nguvu kuliko jeshi la serikali, kwa mujibu wa wachambuzi .

Vijiji hivyo vilitekwa na waasi huku vikosi vya SADEC na MONUSCO vikiwemo mashariki mwa DRC katika kile kinachoitwa "ulinzi wa amani" kwa raia wa taifa hilo.

- Ripoti imeandaliwa na Austere Malivika, Sauti ya Amerika, Goma.

Forum

XS
SM
MD
LG